Mwalimimu Lilian Ndegi
Wito
umetolewa kwa Wanawake Wajawazito,Wakina Mama walio katika Malezi
pamoja na Mabinti kusoma kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kilichoandikwa
na MWL. LILIAN NDEGI wa Kanisa la Living Water Centre chini MTUME ONESMO
NDEGI lililopo Kawe jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania.
Akitoa wito huo katika uzinduzi wa kitabu hicho hivi
karibuni, Mwalimu huyo wa Neno la Mungu Lilian Ndegi amesema kuwa,
kitabu hicho ni msaada mkubwa kwa wakinamama wajawazito kwani watapata
maarifa ya Ki-Mungu yatakayowasaidia kuwaondoa katika uharibifu wa mimba
tangu inapotungwa,inapolelewa,pamoja na wakati wa kujifungua mtoto na
kwamba hiyo inawahusu pia na mabinti ili kuwasaidia kuwa na uzazi mwema
hapo baadae.
Akifafanua zaidi amesema Serikali ya Tanzania imeweka
utaratibu mzuri wa kujenga vituo vya Afya kuwasaidia wakina mama
wajawazito, Mila na Desturi nazo zina kanuni zao, lakini wakati umefika
kwa Kanisa kujihoji Mungu anasema nini juu ya uzao wa Mwenye Haki na
kwamba litembee katika Kanuni zipi ili kuweza kupata ushindi mkubwa
katika Uzazi.
Aidha amesema kitabu hicho kimebeba Ujumbe Wa Mungu
wenye kusudi maalum juu ya maisha ya kiroho na kimwili, utakaofungua
ufahamu wa watu na kuliona Pendo Kuu la Mungu juu ya maisha yao na Uzao
wao maana Mungu anaanza kushughulika na uzao wa Mweye haki kizazi hata
kizazi.
Mwl. Lilian Ndegi ameongeza kuwa kama ambavyo ilikuwa
kwa Ibrahim kupitia kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU,Wazazi na
Walezi kwa ujumla watajifunza mambo muhimu ambayo Mungu anawaagiza
kufanya, kama sehemu ya wajibu wao kwa mfano; Mume kumtunza mkewe siku
zote ,kuwalea na kuwatunza watoto pamoja na kuziona athari za kinywa
katika ulimwengu wa roho zinavyoweza kuathiri maisha ya uzao wao
kutokana na kuwanenea maneno au kuwapa majina yasiyofaa kama vile
kumwita Mtoto Mateso na nk.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Makanisa ya Living Water Center nchini Tanzania Mtume Onesmo Ndegi Mume wa Lilian Ndegi,amewaasa
Wanaume kuwa chachu ya mabadiliko katika ndoa zao, badala ya kujifanya
wana misimamo isiyobadilika, na kuwataka kubadilika wao kwanza katika
mitazamo yao juu ya wake zao na ndipo itakapo kuwa chachu za wake zao
kubadilika kitabia na mienendo katika ndoa.
Aidha
ametoa wito kwa vijana wa kiume kuwa na Mungu zaidi katika ujana wao
ili kumpata Mke Mwema atokae kwa Bwana atakaeweza kuwa msaidizi wa kweli
katika maisha kiroho na kimwili huku akimshukuru Mungu kwa ajili ya Mke
wake Lilian alie mtaja kuwa wa Maana Sana katika maisha yake na
kwamba amefanyika baraka na msaada tosha katika Huduma yake na Familia
kwa ujumla.
Hata hivyo amewataka
wanaume wote kuiga mfano huo wa kuwasifu wake zao na kuwashukuru pamoja
na kuomba msamaha wanapokosea ili ndoa zao zijengwe katika misingi ya
urafiki na penzi la kweli na sio ubabe kama ilivyo miongoni mwa
wanajamii wengi.
Kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kimezinduliwa Jumapili
iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine Mwl. Lilian Ndegi ameelezea kwa
kina juu ya Uzao wa Mwenye Haki,Nalikujua kabla ya Mimba Haijatungwa
Tumboni mwa Mama Yako,Nafasi ya Mwanamume Wakati wa Ujauzito Mpaka
Malezi,Magonjwa na Mateso Mengineyo Katika Kipindi cha Ujauzito,Mtazamo
wa Wazazi juu ya Uzao Wao,Mtazamo wa Mungu juu ya Uzao wa Mwenye
Haki,Mwanamke anahitaji ujasiri Mwingi wakati wa Kujifungua pamoja na
uzazi wa Mpango ndizo sura 8 za kitabu hicho
Hiki ni kitabu cha pili kikitanguliwa na kitabu chake cha kwanza JE
UNASAMEHE? Ambavyo vyote vinapatikana madukani jipatie nakala yako. kwa jumla na rejareja simu nambari 0754465578 au 0655465578 barua pepe lilyonesmo@gmail.com web: www.lwc.or.tz.
Story:Ritha Chuwalo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiy3ggTgV6uTV3d-Zs2iEbyxRZWKI3IrOGGDS5ISZ5qnkdqyYOKzYT8LMIvm_1c2X8vg2U8J7CdqHkOYbvyUy8wtlABrgfs8bc34KIZLga83vQNri2LTjmeCC0J3LCQ0tbV10flEFxhRSo/s1600/2.jpg) |
Apostle Onesmo Ndegi |
|