Huduma ya Living Water Centre, Kawe, imeenea sehemu mbali mbali
Tanzania. Hakika Mungu amekua wa baraka sana kwetu kutuwezesha kueneza
Neno lake. Mikoa tuliopo ni:
Sisi kama kanisa la Mungu, tunaamini na tunaowajibu mkubwa katika kuleta
maisha mapya yenye makusudi yaliyokusudiwa na Mungu mwenyewe kwa
Waaminio katika Familia, Mtu mmoja mmoja, Jumuia, miji na nchi kwa
ujumla. Tunapenda ukweli kwamba, Mungu ni mwaminifu na ahadi zake ni za
kweli, na amekusudia sisi kuwa Chumvi ya ulimwengu, na kupitia sisi,
Watu watauona Mkono wake, na wataufurahia uhalisia wa wema wa Mungu siku
zote za maisha yao. Karibu ujumuike nasi. Mungu Wetu na akubariki sana.