KUISHI MAISHA YA SHIDA NI WEWE UMETAKA, HUITAJI MTU AKUTOLEE NENO LA KINABII--APOSTLE NDEGI

Mtume Onesmo Ndegi - Living Water Centre


Mtume Onesmo Ndegi wa huduma ya Living water Centre Tanzania yenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam,amesema mwanadamu kuishi maisha ya shida na yenye dhiki tele niyeye mwenyewe anajitakia kwakutotaka kubadilika na kufuata sheria ya Mungu.

Mtume Ndegi ameyasema hayo jana usiku wakati wa kipindi kiitwacho ''KWELI IWEKAYO HURU'' kinachorushwa kila siku za ijumaa saa nne kamili usiku kupitia Wapo Radio Fm akiwa sambamba na mtangazaji wa radio hiyo bibie Ritha William Chuwalo ambaye alikuwa akimuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na somo alilokuwa akifundisha.

Akinukuu neno kutoka kitabu cha Luka 10;19 amesema majira tunayoishi sasa siyo ya kuteseka ukizingatia kwamba tumepewa mamlaka ya kumponda kichwa shetani ambaye ndiye chanzo cha maangaiko yote,aidha amesema ukisoma waraka 3 wa Yohana 2 Ni mapenzi ya Mungu kwamba tufanikiwe''Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako,kama vile roho yako ifanikiwavyo''.
amesema Mungu hapendi kuona unateseka na maisha,ndoa,familia,chakula na mambo mengine likiwemo suala zima la fedha.kama ilivyokwa Mungu kwamba anapenda kuona tunafanikiwa ndivyo ilivyo hata kwa mwanadamu kwamba hakuna mtu asiyetaka mafanikio,akasema ila hayo mafanikio chanzo chake kiwe Mungu pekee.


ILI UFANIKIWE UNAHITAJI KUFANYA NINI
Mtume Ndegi amesema kuwa  ili kufanikiwa unahitaji kuwa na ushirika na Mungu,kwakujua neno lake na hayo mengine utazidishiwa,Mungu aliposema roho yako ifanikiwavyo anamaanisha kwa kulijua neno lake na kumjua Mungu suala la kuwa na afya ni mengineyo ambayo tunayapata baada ya kumjua Mungu ambaye ni Roho anayetuwezesha kuzaa matunda kwa wakati muafaka akinukuu kutoka Zaburi 1;1-3

Akatoa mfano kwa mtu anayekwenda sokoni kununua mfano nyanya hawezi kuongezewa asiponunua kwanza,''haiwezekani ufike sokoni umwambie muuzaji kwamba niongeze nyanya wakati hata kununua hujanunua ndivyo hivyo hata kwa Mungu kama humjua vyema kupitia neno lake hakuna kuongezwa'' alisema mtume Ndegi na kumuacha mtangazaji Ritha Chuwalo akimshukuru kwa ufafanuzi huo.
Pia mtume Ndegi alinukuu vifungo kutoka vitabu vya Yohana 4;24, 1Petro 2;2, Yohana 1;14 Wakolosai 3;16.akasema bibilia iko wazi ukitaka ufanikiwe lazima ulijue kwanza,utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa akasema uhitaji mtu akutolee neno la unabii ili ufanikiwe ni wewe mwenyewe juhudi zako za kumtafuta Mungu kwa bidii.

Akasema kazi ya maombi ni kung'oa vifungo vya shetani alivyowafunga watu,pia ni kumkumbusha Mungu ahadi zake kwetu,maana amesema njoo tuhojiane.....pia alinukuu kitabu cha Luka 11;21-26  kinga ya yote ni kuwa na ushirika na Mungu kwa kusoma neno akimtolea mfano Daniel alivyokuwa msomaji wa vitabu na neno na mafanikio yalionekana,Yohana 14;23.

Kanisa la Living water makuti kawe jijini Dar es salaam limeanzisha ibada za maombezi kila siku za Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi na kuendelea ambapo licha ya maombi,Mtume Ndegi amesema kutakuwa na wakati wakujifunza neno la Mungu.


Wiki ijayo ataendelea na somo hili kuanzia saa 4 usiku kupitia Wapo Radio Fm

Pia tunakukaribisha katika Bible study kila Alhamis saa 12:00 jioni Kujifunza Neno kwa mda wa kutosha na kutakuwana wakati wa kuuliza maswali.


Vipindi hivyo vya Wapo Radio Fm unaweza kusikiliza kama uko mbali na mahala Redio inaposikikaa  unaweza kuisikiliza kupitia http://gospelkitaa.blogspot.com na http://samsasali.blogspot.com/
Ijumaa saa 4 usiku.
Jumanne saa 11 jioni



Source:http://gospelkitaa.blogspot.com