Ibada ya Watoto Living Water Centre Makuti Kawe

Ibada ya Watoto Kanisani Living Water Center ni Ibada inayowakutanisha watoto wazazi wao pia na waalimu wa watoto katika kupata mafundisho mbalimbali.

Pia watoto wanapata muda wa kula chakula cha mchana pamoja na michezo mbalimbali katika kufurahi pamoja kwa siku nzima kanisani hapo.

Upande wa zawadi wanazopewa zinakuwa zinatolewa na Father Christmas siku hiyo katika namna ya kuwafurahish watoto na wazazi wao.

Siku ya Jumamosi kanisani hapo huwa ndio siku ya vipindi vya watoto kupata mafundisho na kufahamiana na watoto wenzake.

h[pof[pgof[g

Ephraim Sekeleti ndani ya Living Water Centre Kawe

Ephraim Sekeleti Mutalange ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia na Afrika nzima kwa ujumla,alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia.

Siku ya jana alikuwa katika Kanisa Living WaterCentre Makuti Kawe Dar es salaam chini ya Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi,Ilikuwa ibada ya baraka sana kwa watu walioudhulia katika Ibada hiyo.


Ephraim Sekereti jioni ya leo atakuwa akihudumu katika Ibada ya madhabahu ya Living Water Centre Kawe na pia Living Waters wenyeji watakuwepo kuhudumu.
Ephraim Sekeleti siku ya jana katika madhabahu ya Living Water Centre
Apostle Ndegi,Ephrahim Sekereti na George Mpella
Apostle Ndegi akitamka Neno na mbaraka kwa Ephrahim Sekereti siku ya jana baada ya Kumaliza kuhudumu katika Ibada Living Water Centre.
Ephrahim Sekereti kutoka Zambia siku ya Jana alihudumu katika Ibada Living Water Centre alipata akifanya Korabo na Living Waters.