Mtume Onesmo Ndegi - Living Water Centre
Mtume Onesmo Ndegi wa huduma ya Living water Centre Tanzania yenye makao makuu
yake Kawe jijini Dar es salaam,amesema mwanadamu kuishi maisha ya shida
na yenye dhiki tele niyeye mwenyewe anajitakia kwakutotaka kubadilika na
kufuata sheria ya Mungu.
Mtume Ndegi ameyasema hayo jana usiku wakati wa kipindi kiitwacho
''KWELI IWEKAYO HURU'' kinachorushwa kila siku za ijumaa saa nne kamili
usiku kupitia Wapo Radio Fm akiwa sambamba na mtangazaji wa radio hiyo
bibie Ritha William Chuwalo ambaye alikuwa akimuuliza maswali mbalimbali
kuhusiana na somo alilokuwa akifundisha.
Akinukuu neno kutoka kitabu cha Luka 10;19 amesema majira tunayoishi
sasa siyo ya kuteseka ukizingatia kwamba tumepewa mamlaka ya kumponda
kichwa shetani ambaye ndiye chanzo cha maangaiko yote,aidha amesema
ukisoma waraka 3 wa Yohana 2 Ni mapenzi ya Mungu kwamba
tufanikiwe''Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya
yako,kama vile roho yako ifanikiwavyo''.
amesema Mungu hapendi kuona unateseka na maisha,ndoa,familia,chakula na
mambo mengine likiwemo suala zima la fedha.kama ilivyokwa Mungu kwamba
anapenda kuona tunafanikiwa ndivyo ilivyo hata kwa mwanadamu kwamba
hakuna mtu asiyetaka mafanikio,akasema ila hayo mafanikio chanzo chake
kiwe Mungu pekee.
ILI UFANIKIWE UNAHITAJI KUFANYA NINI
Mtume Ndegi amesema kuwa ili kufanikiwa unahitaji kuwa na ushirika na
Mungu,kwakujua neno lake na hayo mengine utazidishiwa,Mungu aliposema
roho yako ifanikiwavyo anamaanisha kwa kulijua neno lake na kumjua Mungu
suala la kuwa na afya ni mengineyo ambayo tunayapata baada ya kumjua
Mungu ambaye ni Roho anayetuwezesha kuzaa matunda kwa wakati muafaka
akinukuu kutoka Zaburi 1;1-3
Akatoa mfano kwa mtu anayekwenda sokoni kununua mfano nyanya hawezi
kuongezewa asiponunua kwanza,''haiwezekani ufike sokoni umwambie muuzaji
kwamba niongeze nyanya wakati hata kununua hujanunua ndivyo hivyo hata
kwa Mungu kama humjua vyema kupitia neno lake hakuna kuongezwa'' alisema
mtume Ndegi na kumuacha mtangazaji Ritha Chuwalo akimshukuru kwa
ufafanuzi huo.
Pia mtume Ndegi alinukuu vifungo kutoka vitabu vya Yohana 4;24, 1Petro
2;2, Yohana 1;14 Wakolosai 3;16.akasema bibilia iko wazi ukitaka
ufanikiwe lazima ulijue kwanza,utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na
mengine yote mtazidishiwa akasema uhitaji mtu akutolee neno la unabii
ili ufanikiwe ni wewe mwenyewe juhudi zako za kumtafuta Mungu kwa bidii.
Akasema kazi ya maombi ni kung'oa vifungo vya shetani alivyowafunga
watu,pia ni kumkumbusha Mungu ahadi zake kwetu,maana amesema njoo
tuhojiane.....pia alinukuu kitabu cha Luka 11;21-26 kinga ya yote ni
kuwa na ushirika na Mungu kwa kusoma neno akimtolea mfano Daniel
alivyokuwa msomaji wa vitabu na neno na mafanikio yalionekana,Yohana
14;23.
Kanisa la Living water makuti kawe jijini Dar es salaam limeanzisha
ibada za maombezi kila siku za Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi na
kuendelea ambapo licha ya maombi,Mtume Ndegi amesema kutakuwa na wakati
wakujifunza neno la Mungu.
Wiki ijayo ataendelea na somo hili kuanzia saa 4 usiku kupitia Wapo Radio Fm
Pia tunakukaribisha katika Bible study kila Alhamis saa 12:00 jioni Kujifunza Neno kwa mda wa kutosha na kutakuwana wakati wa kuuliza maswali.
Vipindi hivyo vya Wapo Radio Fm unaweza kusikiliza kama uko mbali na mahala Redio inaposikikaa unaweza kuisikiliza kupitia http://gospelkitaa.blogspot.com na http://samsasali.blogspot.com/
Ijumaa saa 4 usiku.
Jumanne saa 11 jioni
Source:http://gospelkitaa.blogspot.com