Kilichojili katika Semina ya Binti na Ufahamu Bora.

Binti na Ufahamu Bora ni semina ya Mabinti inayofanyika kila mwaka katika Kanisa la Living Water Center Kawe,Semina hiyo iliyokuwa ya siku tatu kwa kuongozwa na Mama Lilian Ndegi,Pastor Naomi mhamba na Mwl Rose Mushi, Katika siku ya hitimisho la Semina hiyo siku ya Jumapili Ibada nzima mwanzo hadi mwisho Mabinti ndio walio hudumu.


Semina hiyo ilifunguliwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Center akiwa kama mgeni rasmi,Akizungumza na Mabinti hao aliwaasa katika suala zima la kukimbilia kuwaza kuolewa baadala yake aliwaambia wawaze kuwa na ushirika na Mungu megine yatafuata kwa wakati wake.

Mwl Lilian Ndegi na Pastor Naomi ni wanenaji waliokuwa wazungumza katika semina hiyo ambao ndio wabeba maono ya Semina hiyo kuwa inafanyika kila mwaka Katika kuwaleta mabinti karibu na Mungu ilikuweza kuwaepusha na changamoto za ujana na Dunia kwa ujumla.

Mwl.Rose Mushi pia ni mzungumzaji aliyekwepo  kuzungumza na mabinti katika namna Binti anapaswa kuwa vipi na Jamii anayomzunguka itamtambuaje kwa jinsi alivyo,akaongeza kwa kuzungumzia kanuni za binti anapaswa kuwaje.

Mabinti walipata kujifunza vitu vingi ikiwemo kujitambua na maswala ya mahusiano na changamoto za kimaisha,Semina hiyo ilihitimishwa siku ya Jana Jumapili ikiambatana na Ngoma,Fashion Show amabyo ilidhaminiwa na Mstafa Hassanali,Magizo Dance na kupata muda wa Kusifu na Kuabudu ikiongozwa na Mwl.Rose Mushi.


Pasotr Naomi Mhamba akizungumza na Mabinti

Meza kuu  Katibu wa Living Water Center Ministry Peace Matovu,Mama Apostle Ndegi na Rose Mushi wakifuatilia kwa makini semina.

Mabinti walojitokeza kuuzulia semina hiyo wakifuatilia kwa amakini.

Praise and Worship Team ya mabinti wakihudumu katika Ibada
Edna Luvanda Kiongozi wa Mabinti Kanisani hapo ndio alikuwa MC siku ya hitimishi la semina hiyo.
Apostle Ndegi ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika Semina hiyo.
Wanenaji wa semina hiyo wakifuatilia jambo kwa makini kwa mtumishi wa Mungu Apostle  Ndegi
Semina hiyo ilipambwa na michezo mbalimbali kama ngoma,maigizo,dance na Fashion show kama inavyoonekana.


Baadhi ya Mabinti walioshiriki Fashion Show katika Stage,Nguo walizovaa walidhaminiwa na mbunifu maarufu wa mitindo Nchini Mustafa Hassanali.Magreth Kasanga Mwenyekiti wa mabinti ndiye aliyesimama madhabahuni katika kuhudumu upande wa Neno


Baadhi ya Viongozi wa Mabinti Edina Luvanda,Happiness Kassanga,Happiness Silayo, Grace Mbwiga Mkrugenzi wa Living Water Center katika Pozi.


Mwl. Rose Mushi ndiye aliye kuwa mzungumzaji wa mwisho kwa kutoa mafundisho yenye challange kwa mabinti wenzake kama kawaida yake!