Praise In the City Dar es salaam to Jesus

Ni tamasha la Kusifu na Kuabudu lililoandaliwa na Living Water Centre Kawe lilitakuwa live
Baadhi Waimbaji wote walioimba live (Host) Living Waters Worship TeamJohn Lisu and and TeamGlorious Celebration  Mahali: Diamond Jubilee Hall











VHM wahudumu ndani ya Living Water Centre Kawe











Kilichojili katika Semina ya Binti na Ufahamu Bora.

Binti na Ufahamu Bora ni semina ya Mabinti inayofanyika kila mwaka katika Kanisa la Living Water Center Kawe,Semina hiyo iliyokuwa ya siku tatu kwa kuongozwa na Mama Lilian Ndegi,Pastor Naomi mhamba na Mwl Rose Mushi, Katika siku ya hitimisho la Semina hiyo siku ya Jumapili Ibada nzima mwanzo hadi mwisho Mabinti ndio walio hudumu.


Semina hiyo ilifunguliwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Center akiwa kama mgeni rasmi,Akizungumza na Mabinti hao aliwaasa katika suala zima la kukimbilia kuwaza kuolewa baadala yake aliwaambia wawaze kuwa na ushirika na Mungu megine yatafuata kwa wakati wake.

Mwl Lilian Ndegi na Pastor Naomi ni wanenaji waliokuwa wazungumza katika semina hiyo ambao ndio wabeba maono ya Semina hiyo kuwa inafanyika kila mwaka Katika kuwaleta mabinti karibu na Mungu ilikuweza kuwaepusha na changamoto za ujana na Dunia kwa ujumla.

Mwl.Rose Mushi pia ni mzungumzaji aliyekwepo  kuzungumza na mabinti katika namna Binti anapaswa kuwa vipi na Jamii anayomzunguka itamtambuaje kwa jinsi alivyo,akaongeza kwa kuzungumzia kanuni za binti anapaswa kuwaje.

Mabinti walipata kujifunza vitu vingi ikiwemo kujitambua na maswala ya mahusiano na changamoto za kimaisha,Semina hiyo ilihitimishwa siku ya Jana Jumapili ikiambatana na Ngoma,Fashion Show amabyo ilidhaminiwa na Mstafa Hassanali,Magizo Dance na kupata muda wa Kusifu na Kuabudu ikiongozwa na Mwl.Rose Mushi.


Pasotr Naomi Mhamba akizungumza na Mabinti

Meza kuu  Katibu wa Living Water Center Ministry Peace Matovu,Mama Apostle Ndegi na Rose Mushi wakifuatilia kwa makini semina.

Mabinti walojitokeza kuuzulia semina hiyo wakifuatilia kwa amakini.

Praise and Worship Team ya mabinti wakihudumu katika Ibada
Edna Luvanda Kiongozi wa Mabinti Kanisani hapo ndio alikuwa MC siku ya hitimishi la semina hiyo.
Apostle Ndegi ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika Semina hiyo.
Wanenaji wa semina hiyo wakifuatilia jambo kwa makini kwa mtumishi wa Mungu Apostle  Ndegi
Semina hiyo ilipambwa na michezo mbalimbali kama ngoma,maigizo,dance na Fashion show kama inavyoonekana.


Baadhi ya Mabinti walioshiriki Fashion Show katika Stage,Nguo walizovaa walidhaminiwa na mbunifu maarufu wa mitindo Nchini Mustafa Hassanali.











Magreth Kasanga Mwenyekiti wa mabinti ndiye aliyesimama madhabahuni katika kuhudumu upande wa Neno


Baadhi ya Viongozi wa Mabinti Edina Luvanda,Happiness Kassanga,Happiness Silayo, Grace Mbwiga Mkrugenzi wa Living Water Center katika Pozi.


Mwl. Rose Mushi ndiye aliye kuwa mzungumzaji wa mwisho kwa kutoa mafundisho yenye challange kwa mabinti wenzake kama kawaida yake!

Semina ya Neno la Mungu,Namna Ya Kumiliki Baraka Za Ibrahimu Kibiblia.

Semina ya Neno la Mungu Kuanzia siku ya tarehe 03 October, 2012 mpaka 7 October, 2012 itafanyika katika Kanisa la Living Water Makuti Kawe itafundishwa na Apostle Onesmo Ndegi.

Blog hii iliongea na Apostle ndegi siku ya leo na kutaka kupata ufafanuzi kuhusu semina hiyo. Apostle Ndegi aliongea na kusema ‘Watu Wengi sana hudhani Baraka za Ibrahimu ni zao kama zawadi za father Christmas na Kusahau kuwa kuna Kanuni maalum za kumiliki Baraka hizo zilizo ndani ya Biblia. Tumeona vema wakazi wa Dar-es-Salaam na Vitongozi vyake kujitokeza kusikiliza neno la Mungu na kutamua Kanunuzi za Kumiliki Baraka za Ibrahim Kibiblia kama Mungu alivyoagiza”

Semina hiyo ambayo itafundishwa na Apostle Ndegi Mwenyewe inatazamiwa kuanza rasmi siku ya Kesho na Kuhitimishwa siku ya Jumapili.  Semina itakuwa ikianza Saa 9 na Nusu Jioni.

Apostle Ndegi

Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu


Living Water Centre inakukaribisha katika Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu itakayofanyika Living Water Centre Kawe.
Kuanzia  26/06/2012 uzinduzi Saa 8:00mchana-12jioni, 27-01/06/2012 saa 3:00subuhi-12:00jioni
Watumishi ni
Bishoop Dr Bernard Nwaka-Zambia
Bishop Emanuel Lazaro-Moshi-Tanzania
Apostle Dr Simpson Ngizela - South Africa
Bishop Emmanuel Tumwidike- Mbeya -Tanzania

Wenyeji ni
Apostle Onesmo Ndegi & Lilian Ndegi

Utabarikiwa,Usikose!

Kutembea katika Roho ndani ya TAG na Aposte Ndegi Moshi kwa Askofu Lazaro

Semina ya Neno la Mungu TAG Moshi ikiongozwa na Apostle Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Worship Centre, Katika Semina hiyo ya Siku 5 Apostle Onesmo Ndegi alikuwa akifundisha kuhusu kutembea katika Maisha ya Rohoni,Mwenyeji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi. 
Siku zilikuwa za baraka sana kwa wale walioudhulio udhulia semina hiyo,maana walichokuwa wakifundishwa walikuwa wanakifanyia kazi na kuona matokeo yake.


Mwaka 2012 miezi michache iliyopita Living Water Centre waliandaa semina ya Neno la Mungu Mnenaji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi,Semina hiyo ilikuwa ya Baraka sana kwa watu wengi walioudhulia semina hiyo.Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alibarikiwa na Moyo wa Apostle Onesmo Ndegi jinsi kwa jinsi anavyo fundisha Neno la Mungu,Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alimwandalia Apostle Ndegi semina Moshi kwa makusudi ya kusikiliza Neno kwa kijana wake.

Kama inavyofahamika  kuwa Apostle Onesmo Ndegi amepata Kibali ndani ya moyo wa Bishop Emmanuel Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi, Lazaro ambaye ni Askofu wa Kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.




Apostle Onesmo Ndegi akisistiza jambo wakati wa semina hiyo

Mnamo 26/06/2012 katika Kanisa la Living Water Center Kawe kutakuwa  Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu  ambalo litajumuisha baadhi ya watumishi kutoka Tanzania na nje ya Tanzania Bishop Emmanueli Lazaro ni mmoja wa wanenaji katika Kongamano hilo.Watumishi Wengine watakao hudumu ni pamoja na Bishoop Dr Bernard Nwaka-Zambia,Apostle Dr Simpson Ngizela - South Africa na Bishop Emmanuel Tumwidike- Mbeya -Tanzania..
Baadhi ya waumini wa Kanisa la TAG Moshi kwa Bishop Emmanueli Lazaro wakifuatilia mafundisho kwa makini

Wanakwaya kanisani hapo wakimwabudu Mungu katika Semina hiyo
Kwa Sehemu ndani ya Kanisa umati wa waumini wa Moshi walioudhulia Semina hiyo ya Apostle Onesmo Ndegi katika kanisa la TAG
Maombezi na kufunguliwa pia ilikuwa ni sehemu ya Semina hiyo kama inavyoonekana






Baba na mwana Apostle Ndegi na Askofu Emmanueli Lazaro
Apostle Ndegi, wa pili kulia ni Mchungaji Alex wa Kanisa Living Water Center Moshi,wa tatu ni aliyewahi kujitambulisha kuwa ni kijana Bishop Lazaro,anaye fuatia ni Victor Ishengoma na mwisho ni Mr Rugambage ujumbe aliokuwa ameambatana na kutoka Living Water Centre Dar es salaam