Kutembea katika Roho ndani ya TAG na Aposte Ndegi Moshi kwa Askofu Lazaro

Semina ya Neno la Mungu TAG Moshi ikiongozwa na Apostle Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Worship Centre, Katika Semina hiyo ya Siku 5 Apostle Onesmo Ndegi alikuwa akifundisha kuhusu kutembea katika Maisha ya Rohoni,Mwenyeji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi. 
Siku zilikuwa za baraka sana kwa wale walioudhulio udhulia semina hiyo,maana walichokuwa wakifundishwa walikuwa wanakifanyia kazi na kuona matokeo yake.


Mwaka 2012 miezi michache iliyopita Living Water Centre waliandaa semina ya Neno la Mungu Mnenaji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi,Semina hiyo ilikuwa ya Baraka sana kwa watu wengi walioudhulia semina hiyo.Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alibarikiwa na Moyo wa Apostle Onesmo Ndegi jinsi kwa jinsi anavyo fundisha Neno la Mungu,Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alimwandalia Apostle Ndegi semina Moshi kwa makusudi ya kusikiliza Neno kwa kijana wake.

Kama inavyofahamika  kuwa Apostle Onesmo Ndegi amepata Kibali ndani ya moyo wa Bishop Emmanuel Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi, Lazaro ambaye ni Askofu wa Kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.
Apostle Onesmo Ndegi akisistiza jambo wakati wa semina hiyo

Mnamo 26/06/2012 katika Kanisa la Living Water Center Kawe kutakuwa  Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu  ambalo litajumuisha baadhi ya watumishi kutoka Tanzania na nje ya Tanzania Bishop Emmanueli Lazaro ni mmoja wa wanenaji katika Kongamano hilo.Watumishi Wengine watakao hudumu ni pamoja na Bishoop Dr Bernard Nwaka-Zambia,Apostle Dr Simpson Ngizela - South Africa na Bishop Emmanuel Tumwidike- Mbeya -Tanzania..
Baadhi ya waumini wa Kanisa la TAG Moshi kwa Bishop Emmanueli Lazaro wakifuatilia mafundisho kwa makini

Wanakwaya kanisani hapo wakimwabudu Mungu katika Semina hiyo
Kwa Sehemu ndani ya Kanisa umati wa waumini wa Moshi walioudhulia Semina hiyo ya Apostle Onesmo Ndegi katika kanisa la TAG
Maombezi na kufunguliwa pia ilikuwa ni sehemu ya Semina hiyo kama inavyoonekana


Baba na mwana Apostle Ndegi na Askofu Emmanueli Lazaro
Apostle Ndegi, wa pili kulia ni Mchungaji Alex wa Kanisa Living Water Center Moshi,wa tatu ni aliyewahi kujitambulisha kuwa ni kijana Bishop Lazaro,anaye fuatia ni Victor Ishengoma na mwisho ni Mr Rugambage ujumbe aliokuwa ameambatana na kutoka Living Water Centre Dar es salaam