Mwalimimu Lilian Ndegi akamia Kuukomboa Uzao wa Mwanamke



Mwalimimu Lilian Ndegi 

Wito umetolewa kwa Wanawake Wajawazito,Wakina Mama walio katika Malezi  pamoja na Mabinti kusoma kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kilichoandikwa na MWL. LILIAN NDEGI wa Kanisa la Living Water Centre chini MTUME ONESMO NDEGI lililopo Kawe jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania. 

 Akitoa wito huo katika uzinduzi wa kitabu hicho hivi karibuni, Mwalimu huyo wa Neno la Mungu Lilian Ndegi amesema kuwa, kitabu hicho ni msaada mkubwa kwa wakinamama wajawazito kwani watapata maarifa ya Ki-Mungu yatakayowasaidia kuwaondoa katika uharibifu wa mimba tangu inapotungwa,inapolelewa,pamoja na wakati wa kujifungua mtoto na kwamba hiyo inawahusu pia na mabinti ili kuwasaidia kuwa na uzazi mwema hapo baadae. 

 Akifafanua zaidi amesema Serikali ya Tanzania imeweka utaratibu mzuri wa kujenga vituo vya Afya kuwasaidia wakina mama wajawazito, Mila na Desturi nazo zina kanuni zao, lakini wakati umefika kwa Kanisa kujihoji Mungu anasema nini juu ya uzao wa Mwenye Haki  na kwamba litembee katika Kanuni zipi ili kuweza kupata ushindi mkubwa katika Uzazi. 

 Aidha  amesema kitabu hicho  kimebeba Ujumbe Wa Mungu wenye kusudi maalum juu ya maisha ya kiroho na kimwili, utakaofungua ufahamu wa watu na kuliona Pendo Kuu la Mungu juu ya maisha yao na Uzao wao maana Mungu anaanza kushughulika na uzao wa Mweye haki kizazi hata kizazi.

 Mwl. Lilian Ndegi ameongeza kuwa kama ambavyo ilikuwa kwa Ibrahim kupitia kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU,Wazazi na Walezi kwa ujumla watajifunza mambo muhimu ambayo Mungu anawaagiza kufanya, kama sehemu ya wajibu wao  kwa mfano; Mume kumtunza mkewe siku zote ,kuwalea na kuwatunza watoto pamoja na kuziona athari za kinywa katika ulimwengu wa roho zinavyoweza kuathiri maisha ya uzao wao kutokana na kuwanenea maneno au kuwapa majina yasiyofaa kama vile kumwita Mtoto Mateso na nk.

 Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Makanisa ya  Living Water Center nchini Tanzania Mtume Onesmo Ndegi  Mume wa Lilian Ndegi,amewaasa Wanaume kuwa chachu ya mabadiliko katika ndoa zao, badala ya kujifanya wana misimamo isiyobadilika, na kuwataka kubadilika wao kwanza katika mitazamo yao juu ya wake zao na ndipo itakapo kuwa chachu za wake zao kubadilika kitabia na mienendo katika ndoa.

 Aidha ametoa wito kwa vijana wa kiume kuwa na Mungu zaidi katika ujana wao ili kumpata Mke Mwema atokae kwa Bwana atakaeweza kuwa msaidizi wa kweli katika maisha kiroho na kimwili huku akimshukuru Mungu kwa ajili ya Mke wake  Lilian alie mtaja kuwa wa Maana Sana katika maisha yake na  kwamba amefanyika baraka na msaada tosha katika Huduma yake na Familia kwa ujumla.

 Hata hivyo amewataka wanaume wote kuiga mfano huo wa kuwasifu wake zao na kuwashukuru pamoja na kuomba msamaha wanapokosea ili ndoa zao zijengwe katika misingi ya urafiki na penzi la kweli na sio ubabe kama ilivyo miongoni mwa wanajamii wengi.


Kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU kimezinduliwa Jumapili iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine Mwl. Lilian Ndegi ameelezea kwa kina juu   ya Uzao wa Mwenye Haki,Nalikujua kabla ya Mimba Haijatungwa Tumboni mwa Mama Yako,Nafasi ya Mwanamume Wakati wa Ujauzito Mpaka Malezi,Magonjwa na Mateso Mengineyo Katika Kipindi cha Ujauzito,Mtazamo wa Wazazi juu ya Uzao Wao,Mtazamo wa Mungu juu ya Uzao wa Mwenye Haki,Mwanamke anahitaji ujasiri Mwingi wakati wa Kujifungua pamoja na uzazi wa Mpango ndizo sura 8 za kitabu hicho

                  Hiki ni kitabu cha pili kikitanguliwa na kitabu chake cha kwanza JE UNASAMEHE? Ambavyo vyote vinapatikana madukani jipatie nakala yako.
kwa jumla na rejareja simu nambari 0754465578 au 0655465578 barua pepe lilyonesmo@gmail.com web: www.lwc.or.tz.


 Story:Ritha Chuwalo
                          
Apostle Onesmo Ndegi


Living Waters walihudumu siku hiyo
Ilikuwa furaha sana kwa kwa upande wa akina mama siku hiyo
Watumishi wa Mungu mbalimbali wakitamka Neno na kukiweka wakfu kitabu hicho
Mzee Ernest Tarimo,Mmoja wa watu waliotoa mchango katika uandishi wa kitabu hicho akipokea bahasha ya shukrani siku hiyo
Mmoja wa watu waliotoa mchango katika uandishi wa kitabu hicho ni Dr kwa tahaluma akipokea bahasha ya shukrani siku hiyo

 Apostle Ndegi na Mke wake Lilian Ndegi  wakikata keki
Lilian Ndegi akimlisha keki mme wake Apostle Ndegi kumshukuru lakini pia  kumpongeza kwa kazi kubwa ya kumtia moyo katika kipindi cha uandishi wa kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU
Mtume Onesmo Ndegi akimlisha keki mke wake Lilian Ndegi kumshukuru lakini pia  kumpongeza kwa kazi kubwa ya uandishi wa kitabu cha MUNGU NA UZAO WANGU,sherehe za uzinduzi huo zilifanyika hivi karibuni katika kanisa lao Living Water Center Kawe jijini Dar-es-salaaNa hapa chini ndio picha ya keki yenyewe mfano wa kitabu hicho MUNGU NA UZAO WANGU kabla ya kukatwa.

Mtumishi wa Mungu Rose Mushi alikuwepo katika Uzinduzi huo akiwa ni mmoja wa watu waliohusika katika kitabu hicho kukamilika.
Ritha Chuwalo Mtangazaji wa Wapo Redio FM akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU
Grace Kakiziba akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU
Edna Luvanda Mke wa Antony Luvanda MC maarufu nchini akilishwa keki baada ya kununua kitabu siku hiyo ya uzinduzi wa kitabu hicho cha MUNGU NA UZAO WANGU
Hadson Kamoga akimmiminia Apostle Ndegi Champagne ikiwa ni katika kujipongeza baada ya kuzindua kitabu  cha MUNGU NA UZAO WANGU


 

Wamama wa Living Water Centre na Lilian Ndegi

Mwalimu wa Vijana mwandishi wa Vitabu Rose Mushi akiwa na Mwalimimu Lilian Ndegi
Watumishi wa Mungu kutoka huduma na Makanisa mbalimbali waliokuwepo kuhudhulia uzinduzi huo wa kitabu  cha MUNGU NA UZAO WANGU

Living Water Centre Kawe Katika Uzinduzi wa Logo na Bango Jipya





Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Apostle Onesmo Ndegi

Living Waters Praisse team wakiongoza sifa wakati wa Ibada
Wapiga vyombo vya mziki wa Living Waters Praisse

Bango lenye logo na ujumbe mpya kwa ajili ya mwaka huu 2014