Semina ya Neno la Mungu,Namna Ya Kumiliki Baraka Za Ibrahimu Kibiblia.

Semina ya Neno la Mungu Kuanzia siku ya tarehe 03 October, 2012 mpaka 7 October, 2012 itafanyika katika Kanisa la Living Water Makuti Kawe itafundishwa na Apostle Onesmo Ndegi.

Blog hii iliongea na Apostle ndegi siku ya leo na kutaka kupata ufafanuzi kuhusu semina hiyo. Apostle Ndegi aliongea na kusema ‘Watu Wengi sana hudhani Baraka za Ibrahimu ni zao kama zawadi za father Christmas na Kusahau kuwa kuna Kanuni maalum za kumiliki Baraka hizo zilizo ndani ya Biblia. Tumeona vema wakazi wa Dar-es-Salaam na Vitongozi vyake kujitokeza kusikiliza neno la Mungu na kutamua Kanunuzi za Kumiliki Baraka za Ibrahim Kibiblia kama Mungu alivyoagiza”

Semina hiyo ambayo itafundishwa na Apostle Ndegi Mwenyewe inatazamiwa kuanza rasmi siku ya Kesho na Kuhitimishwa siku ya Jumapili.  Semina itakuwa ikianza Saa 9 na Nusu Jioni.

Apostle Ndegi

Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu


Living Water Centre inakukaribisha katika Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu itakayofanyika Living Water Centre Kawe.
Kuanzia  26/06/2012 uzinduzi Saa 8:00mchana-12jioni, 27-01/06/2012 saa 3:00subuhi-12:00jioni
Watumishi ni
Bishoop Dr Bernard Nwaka-Zambia
Bishop Emanuel Lazaro-Moshi-Tanzania
Apostle Dr Simpson Ngizela - South Africa
Bishop Emmanuel Tumwidike- Mbeya -Tanzania

Wenyeji ni
Apostle Onesmo Ndegi & Lilian Ndegi

Utabarikiwa,Usikose!

Kutembea katika Roho ndani ya TAG na Aposte Ndegi Moshi kwa Askofu Lazaro

Semina ya Neno la Mungu TAG Moshi ikiongozwa na Apostle Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Worship Centre, Katika Semina hiyo ya Siku 5 Apostle Onesmo Ndegi alikuwa akifundisha kuhusu kutembea katika Maisha ya Rohoni,Mwenyeji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi. 
Siku zilikuwa za baraka sana kwa wale walioudhulio udhulia semina hiyo,maana walichokuwa wakifundishwa walikuwa wanakifanyia kazi na kuona matokeo yake.


Mwaka 2012 miezi michache iliyopita Living Water Centre waliandaa semina ya Neno la Mungu Mnenaji alikuwa ni Bishop Emmanueli Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi,Semina hiyo ilikuwa ya Baraka sana kwa watu wengi walioudhulia semina hiyo.Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alibarikiwa na Moyo wa Apostle Onesmo Ndegi jinsi kwa jinsi anavyo fundisha Neno la Mungu,Baada ya hapo Bishop Emmanueli Lazaro alimwandalia Apostle Ndegi semina Moshi kwa makusudi ya kusikiliza Neno kwa kijana wake.

Kama inavyofahamika  kuwa Apostle Onesmo Ndegi amepata Kibali ndani ya moyo wa Bishop Emmanuel Lazaro wa Kanisa la TAG Moshi, Lazaro ambaye ni Askofu wa Kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.




Apostle Onesmo Ndegi akisistiza jambo wakati wa semina hiyo

Mnamo 26/06/2012 katika Kanisa la Living Water Center Kawe kutakuwa  Kongamano la Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu  ambalo litajumuisha baadhi ya watumishi kutoka Tanzania na nje ya Tanzania Bishop Emmanueli Lazaro ni mmoja wa wanenaji katika Kongamano hilo.Watumishi Wengine watakao hudumu ni pamoja na Bishoop Dr Bernard Nwaka-Zambia,Apostle Dr Simpson Ngizela - South Africa na Bishop Emmanuel Tumwidike- Mbeya -Tanzania..
Baadhi ya waumini wa Kanisa la TAG Moshi kwa Bishop Emmanueli Lazaro wakifuatilia mafundisho kwa makini

Wanakwaya kanisani hapo wakimwabudu Mungu katika Semina hiyo
Kwa Sehemu ndani ya Kanisa umati wa waumini wa Moshi walioudhulia Semina hiyo ya Apostle Onesmo Ndegi katika kanisa la TAG
Maombezi na kufunguliwa pia ilikuwa ni sehemu ya Semina hiyo kama inavyoonekana






Baba na mwana Apostle Ndegi na Askofu Emmanueli Lazaro
Apostle Ndegi, wa pili kulia ni Mchungaji Alex wa Kanisa Living Water Center Moshi,wa tatu ni aliyewahi kujitambulisha kuwa ni kijana Bishop Lazaro,anaye fuatia ni Victor Ishengoma na mwisho ni Mr Rugambage ujumbe aliokuwa ameambatana na kutoka Living Water Centre Dar es salaam

MARRIAGE WORKSHOP NA CHAKULA CHA JIONI

Marriage Workshop hiyo ilipambwa na mafundisho ya tofauti yakiongozwa wamtumishi wa Mungu, Mtume Onesmo Ndegi na Mwl Lilian Ndegi kuhusu watu walio katika Kristo Yesu maisha yao yanapaswa kuwa vipi,Usiku huo pia uliudhuliwa na watu mbalimbali wake kwa waume,pia mzazi mmoja mmoja,vijana walijitokeza kwa kiasi kikubwa kwa kile kilicho dhaniwa kuwa ni kupata mafundisho kwa ajili ya maandalizi ya maisha yao ya baadae kabla ya ndoa.

Jioni hiyo pia ilikuwa ni Marriage Anniversary ya Mtume Onesmo Ndegi na Mwl Lilian Ndegi hivyo usiku huo kulikuwa na kufungua Champagne pia kukata keki kwa ajili ya watumishi wa Mungu hao na chakula cha pamoja kwa wote.

Baadhi ya wanandoa walipata kuuliza maswali kuhusu changamoto wanazo kutana nazo katika ndoa.



Mtume Ndegi na Lilian Ndegi 

Wanandoa walioudhulia ndoa hiyo wakifuatilia mafundisho katika tukio hilo







Pastor Naomi Mhamba akitoa ushuhuda kuhusu Maisha yake ya Ndoa  


LIFE TRANSFORMATION COURSE WAFANYA GRADUATION YA KUHITIMU DARASA HILO.


Kwa mara nyingine tunashuhudia wanafunzi wa  8th Graduation ya Life Transforming Course, wakihitimu darasa la utumishi walilokuwa wakisoma kwa kipindi cha miezi mitatu katika kukulia wokovu,Baadhi ya wanafunzi wakizungumza kuhusiana na darasa hilo wamesema limekuwa la msaada sana.Hasa wengine wameokoka lakini baada ya kusoma darasa hilo kwa vitu walivyo vipata vimewafanya wajione kama hapo mwanzo walikuwa hawajaokoka!

Katika darasa hilo la utumishi Mkuu wa chuo hicho Mtume Onesmo Ndegi akishilikiana na Mwalimu Lilian Ndegi pia Naomi Mhamba na wengine wengi ni miongoni mwa watumishi wa Mungu walio hakikisha darasa hilo linafayika kama ilivyo pangwa.



Baadhi ya wanafunzi hao wakioongoza sifa siku ya sherehe hiyo.


 Wahitimu wa darasa la utumishi kama wanavyoonekana katika picha wakati mahafari hayo yakiendelea kanisani.


Mmoja wa wahitimu akitoa ushuhuda kuhusiana na darasa hilo la utumshi
Ritha Chuwalo alikuwa mmoja wa wnafunzi hao akitoa ushuhuda wakati wa Ibada
Mwanafunzi aliye semekana kuwa ni mdogo kuliko wote katika darasa hilo akisoma risala ya darasa .
Mtume onesmo ndegi akijibu risala ya waitimu

Baadhi ya mwanafunzi wakipokea zawadi za kufanya vizuri katika kozi hiyo kutoka kwa Mtume Onesmo Ndegi


Miongoni mwa michezo walioicheza ni pamoja na ngoma





MARRIAGE WORKSHOP DINNER

Marriage Workshop Dinner.
19/May/2012
Huduma ya Living Water Centre Kawe inakualika
Katika Marriage Workshop itakayo ambatana na Mafundisho ya ndoa pia Chakula cha jioni.
Picolo Hotel Kawe.
Couple 50,000/= Single 30,000/=
Kuanzia saa 12:00 jioni - saa 3:00 usiku

Karibu
sana na Mungu akubariki 

Mawasiliano:
0784 580400
0655 391664
0766 802390












LIVING WATER CENTRE KIMALA KATIKA IBADA YA SHUKRANI



Mtume  Onesmo Ndegi alikuwepo kama mgeni rasmi katika ibada hiyo.

Pastor Angela Kibaja ambaye ndiye mwenyeji wa kanisa la Living Water Centre Kimala



 Baadhi ya watu walioudhulia ibada hiyo kutoka ibada hiyo kutoka makanisa mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwepo Living Water Center Kawe


Mchungaji Paschal Mnemwa wa Huduma ya Living Water Centre-Kibaha na Mchunga Devota Gwao wa huduma ya Living Water Centre-Kitunda wakwanza kulia wakifuatilia Neno kwa umakini kutoka kwa mtumishai wa Mungu.
Kikundi cha Sifa kutoka Kanisa la Kitunda ndicho kilichoongoza sifa siku hiyo

Mchunga Devota Gwao wa huduma ya Living Water Centre-Kitunda akiongoza sifa

Baadhi ya watu walioudhulia ibada hiyo



Mwisho wa Ibada kulikuwa na vinywaji na kubadilishana mawazo hapa na pale
Baada ya chakula cha kiroho kilifuatiwa na chakula cha mwilini vinywaji mbalimbali vilikuwepo katika kukamilisha ibada hiyo.

Watenda kazi wa Bwana waliofanikisha ibada hiyo Christina na Doroth Kibaja

KONGAMANO (WARSHA ) YA MWANAMKE WA HEKIMA

Umoja wa wamama wa Living Water Centre wanakukaribisha katika Kongamano (warsha) ambayo imelenga kumgusa mwanamke mmoja mmoja wahali yoyote katika maisha walengwa ni  (Wanandoa,Wajane,Single Mothers, Mabinti)imelenga kujitambua nakuishi maisha yaushindi katika mazingira ya hali yoyote aliyopo.

Waalimu mahili wapakwa mafuta wa Bwana watakuwepo wakiongozwana Mwl Lilian Ndegi.

HAKUNA KIINGILIO,WOTE MNAKARIBISHWA

Kwamawasilianozaidi;

0784 880400
0655 391664
0766 802390



KUISHI MAISHA YA SHIDA NI WEWE UMETAKA, HUITAJI MTU AKUTOLEE NENO LA KINABII--APOSTLE NDEGI

Mtume Onesmo Ndegi - Living Water Centre


Mtume Onesmo Ndegi wa huduma ya Living water Centre Tanzania yenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam,amesema mwanadamu kuishi maisha ya shida na yenye dhiki tele niyeye mwenyewe anajitakia kwakutotaka kubadilika na kufuata sheria ya Mungu.

Mtume Ndegi ameyasema hayo jana usiku wakati wa kipindi kiitwacho ''KWELI IWEKAYO HURU'' kinachorushwa kila siku za ijumaa saa nne kamili usiku kupitia Wapo Radio Fm akiwa sambamba na mtangazaji wa radio hiyo bibie Ritha William Chuwalo ambaye alikuwa akimuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na somo alilokuwa akifundisha.

Akinukuu neno kutoka kitabu cha Luka 10;19 amesema majira tunayoishi sasa siyo ya kuteseka ukizingatia kwamba tumepewa mamlaka ya kumponda kichwa shetani ambaye ndiye chanzo cha maangaiko yote,aidha amesema ukisoma waraka 3 wa Yohana 2 Ni mapenzi ya Mungu kwamba tufanikiwe''Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako,kama vile roho yako ifanikiwavyo''.
amesema Mungu hapendi kuona unateseka na maisha,ndoa,familia,chakula na mambo mengine likiwemo suala zima la fedha.kama ilivyokwa Mungu kwamba anapenda kuona tunafanikiwa ndivyo ilivyo hata kwa mwanadamu kwamba hakuna mtu asiyetaka mafanikio,akasema ila hayo mafanikio chanzo chake kiwe Mungu pekee.


ILI UFANIKIWE UNAHITAJI KUFANYA NINI
Mtume Ndegi amesema kuwa  ili kufanikiwa unahitaji kuwa na ushirika na Mungu,kwakujua neno lake na hayo mengine utazidishiwa,Mungu aliposema roho yako ifanikiwavyo anamaanisha kwa kulijua neno lake na kumjua Mungu suala la kuwa na afya ni mengineyo ambayo tunayapata baada ya kumjua Mungu ambaye ni Roho anayetuwezesha kuzaa matunda kwa wakati muafaka akinukuu kutoka Zaburi 1;1-3

Akatoa mfano kwa mtu anayekwenda sokoni kununua mfano nyanya hawezi kuongezewa asiponunua kwanza,''haiwezekani ufike sokoni umwambie muuzaji kwamba niongeze nyanya wakati hata kununua hujanunua ndivyo hivyo hata kwa Mungu kama humjua vyema kupitia neno lake hakuna kuongezwa'' alisema mtume Ndegi na kumuacha mtangazaji Ritha Chuwalo akimshukuru kwa ufafanuzi huo.
Pia mtume Ndegi alinukuu vifungo kutoka vitabu vya Yohana 4;24, 1Petro 2;2, Yohana 1;14 Wakolosai 3;16.akasema bibilia iko wazi ukitaka ufanikiwe lazima ulijue kwanza,utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa akasema uhitaji mtu akutolee neno la unabii ili ufanikiwe ni wewe mwenyewe juhudi zako za kumtafuta Mungu kwa bidii.

Akasema kazi ya maombi ni kung'oa vifungo vya shetani alivyowafunga watu,pia ni kumkumbusha Mungu ahadi zake kwetu,maana amesema njoo tuhojiane.....pia alinukuu kitabu cha Luka 11;21-26  kinga ya yote ni kuwa na ushirika na Mungu kwa kusoma neno akimtolea mfano Daniel alivyokuwa msomaji wa vitabu na neno na mafanikio yalionekana,Yohana 14;23.

Kanisa la Living water makuti kawe jijini Dar es salaam limeanzisha ibada za maombezi kila siku za Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi na kuendelea ambapo licha ya maombi,Mtume Ndegi amesema kutakuwa na wakati wakujifunza neno la Mungu.


Wiki ijayo ataendelea na somo hili kuanzia saa 4 usiku kupitia Wapo Radio Fm

Pia tunakukaribisha katika Bible study kila Alhamis saa 12:00 jioni Kujifunza Neno kwa mda wa kutosha na kutakuwana wakati wa kuuliza maswali.


Vipindi hivyo vya Wapo Radio Fm unaweza kusikiliza kama uko mbali na mahala Redio inaposikikaa  unaweza kuisikiliza kupitia http://gospelkitaa.blogspot.com na http://samsasali.blogspot.com/
Ijumaa saa 4 usiku.
Jumanne saa 11 jioni



Source:http://gospelkitaa.blogspot.com

EPHLAHIM SEKELETI AKIHUDUMU LIVING WATER CENTER SIKU YA JUMAPILI

Eprahim Sekereti akihudumu katika Ibada madhabahuni Living Water Centre-Kawe

Hapa alikuwa akifanya collaboration na Living Waters wenyeji.

     


Aposlte Ndegi Liliani Ndegi na baadhi ya Viongozi wa Living Water Centre wakifuatilia jambo kwa makini.

Aposle Ndegi na Eprahim Sekereti

Apostle Ndegi,Eprahim Sekereti,George Mpella kama wanavyoonekana kwenye picha,Living Water Kawe baada ya Ibada.

IBADA YA MAOMBEZI NA UKOMBOZI KWA WATOTO

 Ibada  ya ukombozi na maombezi kwa Watoto ilifanyika siku ya tarehe 14/01/2012 Jumuamosi kanisani Living Water Center Kawe,kwa kuongozwa na Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi akishilikiana na wachungaji pia watendakazi katika kuifanikisha ibada hiyo.
Katika ibada hiyo watoto kwa kiasi kikubwa walifunguliwa na kuponywa ila asilimia kubwa ya watoto wengi wameonekana kuwa wameshambuliwa na kuvamiwa na roho mbalimbali za hasira,uchungu uzito wa akili na nyingine nyingi bila ya wazazi wao kuwa wanajua kinacho wakabili watoto wao nawengine kubaki wakishangaa kilichokuwa kinaendelea katika ibada hiyo
Ibada hiyo iliyoonekana kuwa ni ndefu na kuonekana kurudiwa Jumamisi ijayo siku ya tarehe 21/01.2012.Wazazi wameshauliwa kuja na watoto wao kwa wingi bila kukosa.
Karibu pia nawewe na Utabarikiwa!


Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi alipo kuwa akifundisha wakati wa Ibada hiyo.



Watoto walikuwa wakiombewa kama inavyoonekana kwenye picha


                                                            Watoto walikuwa wakiombewa


Mtume Onesmo Ndegi Alikuwa akiwapaka watoto  mafuta na kuwaombea mmoja mmoja katika ibada hiyo

Wengine walikuwa wakiombewa na kufunguliwa kwa mda mrefu kutokana na matatizo waliyokuwa nayo.

Pia kuzungumza na watoto kwa ukaribu na upole ulifanyika kama anyoonekana Dr,Mchungaji  Mhamba

Kwa jina la Yesu mapepeo yaliondoka tu!

Mapepeo yakitolewa kwa saaaaaana


Watoto wadogo na wazazi  wao waliombewa


Maomezi na Kufunguliwa kwa sana